“SHIMIWI” – Shirikisho limeanzishwa kwa Mujibu wa Sheria Na. 12 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake Sheria Na. 6 ya mwaka 1971 “The National Sports Council of Tanzania Act, 1967”. Michezo ya Watumishi wa Serikali imeanzishwa toka enzi za ukoloni, lakini Shirikisho hili limesajiliwa rasmi na Msajili wa Vilabu na Vyama vya Michezo tarehe 21 Novemba, 1984 kwa jina la “Inter-ministerial Sports Organization” (ISO). Tarehe 18 Agosti, 2010, Shirikisho likajisajii kwa jina la Kiswahili

Habari za Matukio mbali mbali

Mission

  1. Kuwakutanisha wafanyakazi wa Wizara, Idara, Mikoa na Wakala wa Serikali bila kujali kada ,jinsia,rangi au dini zao katika michezo.
  2. Kukuza, kusimamia na kuongoza michezo na mashindano kati ya wanahama wake, vilabu vya michezo mbalimbali, mashirikisho mengine chini hata nje ya nchi kulingana na hali itakavyoruhusu.
  3. Ushirikishwaji wa wafanyakazi katiaka michezo kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya ya mwili na akili.
  4. Kujenga na kuendeleza tabia ya ushirikiano, upendo na udugu baina ya Mfanyakazi na Mfanyakazi kutoka katika Wizara, Idara, Mikoa na Wakala.
  5. Kufanya mengine yoyote ambayo yatakuwa na manufaa na yenye kuendeleza michezo kwa wanachama na kwa umma kwa jumla.